Jini Kabula aeleza familia yake ilivyomtemga baada ya kuugua ugonjwa wa akili

Miriam Jolwa anayetambulika Kama Jini Kabula ni muigizaji aliyepata umaruufu kupitia tamthiliya ya Jumba la Dhahabu. Hata hivyo kwa hivi sasa anaonekana hali ya akili haiko sawa.

Baada ya Wolper kujitokeza na kuwaomba wasanii wenzake kumsaidia Jini, Global TV online iliweza kukutana na yeye Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo walizungumza na yeye na kulingana na walichotangaza, ni kweli Jini anapitia wakati mgumu.

download latest music    

Mrembo huyu alifunguka kudai kuwa wetu ana tatizo kwenye akili yake na akaendelea kukiri kuwa ndugu zake walimpeleka Muhimbili ambako alilazwa kwenye wodi ya wagonjwa akili kwa zaidi ya mwezi mmoja na kumtenga.

Kwa Sasa hana sehemu ya kuishi na ndugu, jamaa na marafiki zake, wamemtenga kutokana na matatizo aliyonayo na kumbidi kutangatanga mitaani.

Tazama mahojiano yao hapa;

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua