Jini Kabula Afungukia Ndoa Ya Zabibu Kiba na Aliyekuwa Mpenzi Wake

Muigizaji wa Bongo movie Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka na kuweka wazi kuwa hana tatizo na Zabibu Kiba kufunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake mchezaji wa mpira Abdul Banda.

Siku za nyuma Jini Kabula na mchezaji wa Timu ya Baroka iliyopo Afrika Kusini, Abdul Banda waliwahi kuwa Kwenye uhusiano wa kimapenzi lakini hivi sasa Abdul yuko na Mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba, Zabibu Kiba na wapo mbioni kufunga ndoa.

download latest music    
                               Jini Kabula

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Jini Kabula alisema anawashangaa baadhi ya watu wanaomshambulia kwa maneno machafu kwenye mitandao ya kijamii kisa aliwahi kuwa na uhusiano na Banda lakini hawakufanikiwa kuingia kwenye ndoa kitu ambacho ni kawaida tu katika maisha.

Kwanza nafurahi sana Zabibu kuele­kea kwenye ndoa na Banda nawaombea ifanyike salama na sina kinyongo hata kidogo lakini kuna hawa vizabizabina vya pembeni vinaleta chokochoko na kusema eti nilishindwa kuolewa mimi, niwaambie tu kwamba siyo kila mtu unapokuwa naye kwenye uhusiano lazima muoane hivyo waache kuongea mambo wasiyoyajua“.

Zabibu yupo katika shamrashamra za kuelekea Kwenye ndoa ambapo siku chache zilizopita alionekana akifanyiwa visomo mbali mbali na inasemekana kuwa harusi yaweza kuwa muda wowote.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.