Joel Lwaga Aomba Radhi kwa Mama Muna

Msanii wa muziki wa injili Joel Lwaga amempigia simu mama mzazi wa Muna love na kumuomba msamaha kwa yote yalitokea katika msiba wa mtoto wa Muna aitwae Patrick na kumuomba mama huyo kuyaongea na kuyamaliza pale watakapomaliza msiba.

Joel ambae lengo lake kubwa la kupiga simu ilikuwa ni kuomba msamaha kwa mama huyo kwa kuwa na mahusiano ya kimapezni na muna huku akisema kuwa hakuwahi kujua swala la Muna kuwa aliwahi kuolewa ndoa ya kanisani na ndoa hiyo haijavunjika na kuwa inatambulika kisheria.

download latest music    

Baada ya kupatikana kwa habari hizo, kampuni ya habari ya GPL waliamua kumtafauta mama mzazi wa Muna ili kuhakikisha swala hilo ndipo mama alipokubali kuwa alishapigiwa simu na msanii huyo lakini alikataa kusema waliongea nini.

Siwezi mimi kuongea chochote sasa hivi lakini ni kweli kuwa alipiga simu ila siwezi kuweka wazi kitu chochote kwa sasa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.