Joh Makini aeleza umuhimu wa kuachia audio kali badala ya kutumia hela mingi kwenye video

Imefika wakati ambapo Watanzania wameanza kurudi kisikiza audio badala ya kuangalia video za muziki kulingana na alichosema Joh Makini ambaye ni rapa mkali kutoka Tanzania.

download latest music    

Msanii huyu alisisitiza kuwa kuna umuhimu w kuachia audio kali atakama video yake haitakuwa imefika kiwango cha kuridhisha. Msanii huyu aliambia E-Newz ya EATV kuwa muziki ni audio na ikiwa mtu anapanga kufanya vizuri inabidi ajikaze kwenye mistari yake.

Msanii huyu alipeana mfano wa hapo zamani ambapo wasanii wengi hawakuwa wakitengeneza video kali ilhali audio zao zilikuwa zinafanya vyema, Joh alisema,

“Baadae ilipoanza mambo ya video ikawa hata mtu akitoa wimbo na video kali wimbo unakuwa mkubwa. Baadae Watanzania walipoacha kushangaa picha, imekuja wakati ukipiga video kali kama wimbo ni wa kawaida hautoki, kwa hiyo cycle ni ile ile, wimbo ni audio kwanza haijalishi video kubwa au ndogo kwa hiyo ngoma kama ni kali kwenye audio inafanya chochote.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua