Joh Makini Ataja Sababu Za Kutoa Wimbo Wa Gospel

Staa wa muziki wa Hip Hop Bongo Joh Makini maarufu kama Mwamba wa Kaskazini kutokea kundi la Weusi amefunguka na kutaja sababu zilizomsukuma kutoa wimbo wa Injili.

Joh Makini amesema sababu kubwa iliyomfanya mpaka kuimba wimbo wa gospel ni kuonyesha ni Kwa jinsi gani Mungu ana maana kubwa maishani mwake.

download latest music    

Kwenye mahojiano na gazeti la  Risasi Vibes, Joh Makini alisema kwamba wimbo huo kwake ni ‘Hip Hop Gospo’ wenye ujumbe ‘strong’ na si mwisho wa kuimba nyimbo za namna hiyo, ataendelea kila anapopata idea kwa sababu Mungu ni kila kitu kwake.

Hakuna ambaye hafahamu kwamba Mungu ni kila kitu kwenye maisha ya binadamu, nimeimba wimbo huu ili kufikisha ujumbe kwa mashabiki zangu kufahamu kwamba suala la Mungu kutufanikisha kwenye maisha yetu si la kumwachia yeye tu. “Sisi pia tunatakiwa kupambana kwa namna zetu nay eye anabariki nia zetu na kufanya tupate kila tunachotamani”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.