Joh Makini- Mimi ni Tofauti Ya Wasanii Wote Bongo

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya Hip hop Joh Makini ‘Mwamba wa Kaskazini’ amefunguka na kudai kuwa yeye ni msanii tofauti sana na wa kipekee ukilinganisha na wasanii wengine wote Bongo.

Rapa kutoka kundi la Weusi amesema tungo anazozitumia kwa sasa kwenye muziki wake ni kutokana na mabadiliko ya muziki na anaonyesha sanaa zaidi kwenye nyimbo zake na kusisitiza kuwa anayetaka kumfatilia afuatilie mziki wake kwa kuwa maisha yake binafsi hayamhusu na wala yeye sio mtu wa show-off.

download latest music    

Job Makini amefunguka hayo na zaidi kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kupitia kipindi chao cha Enews:

My personal life style ni my personal life style sipendi kuweka kwenye media ninachokiweka kwenye media ni hii sura ya Joh Makini brand ya Joh makini basiii na ninafanya hivyo sio kwamba labda kuna kitu nahofia hapana hivi ndivyo mimi nilivyo Joh Makini ndio yuko hivi nipo tofauti na wasanii wengine wote. Mimi nafanya mziki mzuri nawapa mashabiki zangu lakini maisha yangu binafsi hakuna mtu anayehitaji kujua wala sidhani kama kuna mtu namnyima haki kwa kufanya maisha yangu binafsi tabaki kuwa binafsi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.