Johari Afunguka Kuhusu Kukaa Kimya Baada Ya Hukumu Ya Lulu,Amwaga Chozi

Watu wengi walimposti katika mitandao ya kijamii ikiwa ni kama njia ya kuonyesha  na kuguswa kwao na  machungu yao baada ya Lulu kuhukumiwa kifungo cha miaka mwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia katika mauaji ya msanii aliyekuwa maarufu ndani na nje ya Tanzania marehemu Steven Kanumba.Lakini wapo baadhi ya watu wa karibu kabisa ambao hawakutaka kuonyesha kitu chochote katika jamii , mmoja wapo ni Johari Chagula.

johari chagula amabe pia ni msanii wa bongo movies alikuwa ni mtu wa karibu kabisa na marehemu kwa sababu walikuwa wmetoka mkoa mmoja na walikuwa wakishirikiana karibia katika kila hali na marehemu, yeye pia hakutaka kupost kitu chochote katika mitandao ya kijamii anayojihusisha nayo, hata hivyo alipoulizwa johari hakusita kufunguka kile alichokuwa nacho moyoni.

download latest music    

Johari anasema kuwa sio kila ananepost basi ni kweli anakuwa na maumivu ya kile kilichotokea wengine wanapost tu ili kuonyesha wameguswa lakini laa, lakini pia sio lazima kila maumivu yake ayaonyeshe kwa watu kuwa ameumia inawezekana akawa ameumia lakini ameamua kuvumulia moyoni mwake mwenyewe.

Nadhani kama mtu kitu kinakuuma zaidi unaweza ukakaa tu ukawa unaumia na nafsi yako,sio umuonyeshe kila mtu au uanze kuposti,na sio kwamba nikiweka katika instgram basi yule mdogo wangu vinaweza kumfikia na akajua kuwa johari ameniposti zaidi sana itakuwa inaongeza vitu vingi kwa jamii na kumuumiza na kuniumiza zaidi ndani ya moyo wangu.Huzuni yangu iko ndani ya moyo wangu

Kuguswa nimeguswa sana kwa sababu mimi nipo pande zote mbili , Lulu ni mdogo wangu ameazna tuko nae wote pale kaole, na Kanumba ni kaka angu tuetoka wote Shinyanga nyumbani, kwaio kuguswa nimeguswa sana lakini kinapokuja kitu kama hiki sio lazima nikaposti ili kila mtu nae ajue kuwa nimeguswa au nimeumia sana.wengine labda wamepsti ila wamepost unafiki tu.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu kauli ya baba wa marehemu kuhusu kuwa hukumu hiyo ni ndogo sana , Johari anasema kuwa baba anatakiwa ashukuru Mungu tu kwa sababu haujui kesho yako , tunachopaswa ni kuwa na imani tu na sio kitu kingine.

Baba atambue kuwa Kanumba alikuwa mwanae lakini pia hata Lulu pia ni mwanae kwaio ningemuomba tu aweke imani yake mbele na kumuomba Mungu kwa sabbau ukisema hukumu haikumstaili wakati hata angepewa miaka kumi na akaimaliza miaka yake akirudi anakuwa huru bado.- Alimalizia Johari

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.