Johari Kufanya Maombi Baada Ya Kuandamwa na Mikosi

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Johari Chagula ameibuka na kudai kuwa ana Mpango wa kufanya maombi maalumu kwa ajili kuondoa mkosi ambao amedai umekuwa ukimuandama.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Johari ameibuka na kudai ameamua kufanya maombi maalumu kutokana na mikosi ambapo amesema mwezi uliopita aliibiwa, alipata ajali ya gari hivyo kwake anaona si kawaida kwa hiyo anamuomba Mungu amuepushe na mabalaa ili aweze kumaliza mwaka vizuri.

download latest music    

Ulikuwa mwezi mgumu kwangu, nimepitia kwenye changamoto za mfululizo lakini namshukuru Mungu nipo imara. Nafanya maombi maalum Mungu aniepushe na mabalaa”.

Lakini pia mbali na kupatwa na majanga hayo mwezi uliopita kuna picha ziisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha akiwa amelewa chakari na taarifa kusambaa kwamba kwa hivi sasa ana tatizo la kunywa pombe kupindukia.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.