Johari:-Sijawahi Kugombana na Chuchu kwa Sababu ya Ray

Mwanadada mkongwe katika tasnia ya bongo movie Jahari  Blandina Chagula amefunguka na kuzungumzia swala lililokuwa limesambaa kwa muda mrefu kuhusu yeye kugombana na Chuchu Hans kwa sababu ya ray na hawajawahi kugombana kabisa.

Johari ambae ilisemekana kuwa na mahusiano ya kimapezni na Ray kwa muda mrefu na kutengeneza kampuni ya uzalishaji wa filamu nchini ya RJ Company , aligombana na mwanamke mwenzake baada ya kusikia kuwa Chuchu Hans anatoka kimapenzi na Ray ambae alikuwa mpenzi wake yeye hivyo kutaka hata kuvunja kampuni ambayo ilikuwa ni ya umoja wao.

download latest music    

Akikanusha tetesi hizo katika Kikaangoni live ya EATV, Johari anasema kwa “Sijawahi kugombana na mtu yoyote, na sijawahi kugombana na chuchu kwa sababu ya ray, na hata tangu niingie kwenye sanaa siajwahi kugombana na msanii mwenzake hata mara moja.’

Uwezi kuzuia watu kuongea lakini sijawahi kugombana na mtu yoyote na hata siwezi kuzungumzia maswala ya watu, kwa sababu niko hapa kuzungumzia kazi zangu na sio kuzumgumzia watu wengine.

Hivi unavyoniona mimi nina muda wa kugombana kweli, na kwanini mimi nichukie Chuchu anapotoka na Ray. mimi sikuwahi kujuaswala la mimi kutembea na ray na hizo tetezi ni za uongo.Mimi na Ray hatujawahi kuwa wapenzi hata mara moja kwanza unavyoniuliza natumia nguvu nyingi kuelezea maisha ya watu wengine , sipendi kuongelea hivyo vitu.

Kwa kumaliza johari alikataaa kujibu maswali yote ambayo aliulizwa kuhusu mahusiano yake na ray, na hata kuongelea kuhusu Chuchu Hans.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.