Jokate Afunguka Baada Ya Kuteuliwa Kuwa Mkuu wa Wilaya

Mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006-2007 Jokate Mwegelo amefunguka rasmi baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya siku ya Jumamosi.

Jokate ameteukiwa kuwa mkuu wa wilaya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Pombe Magufuli mwishoni mwa wiki iliyopita.

download latest music    

Baada ya kupata nfasi hiyo Jokate amefunguka mazito ambapo ameweka wazi kuwa mwaka jana tu alikuwa Kwenye hatua za kukata tamaa Kwenye mambo ya siasa.

Jokate amesema mwaka jana alitaka kukata tamaa kwenye maisha yake ya siasa kwani aliona giza mbele yake lakini hakufanya hivyo hii ni kutokana na kupokea maoni mengi kutoka kwa vijana ambao alikuwa anawashawishi kuingia kwenye siasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jokate ameandika:

Amini Mungu ni mwingi wa rehema kamwe hamtupi amtumainiye yeye!! Ahsante Mungu Wangu. Labda ni-share kitu kidogo, kuna muda mwaka jana mwishoni nilikuwa so down nilitamani kukata tamaa na kila kitu kwenye maisha nilikuwa pia sijaelewa vizuri hatma yangu kwenye siasa. Nilikuwa kwenye mkutano mkuu wa chama kuna mdada mmoja kutoka Arusha akanikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu sana alikuwa na mama mmoja hivi walikuwa wamekuja kupiga picha namimi.

Huyo dada mdogo hivi akasema ananipenda sana sana na mimi ndio nilimfanya aingie kwenye siasa na akagombea nafasi kupitia mkoa wa Arusha akashinda!! Nikabaki natabasamu. Ikanipa nguvu kubwa ya kupiga moyo konde na kusonga mbele. Nilifurahi kuona kuna mdada nimeweza kumhamasisha na kumpa ujasiri wa kugombea. Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako lakini inakubidi usikate tamaa saa zingine kwasababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako.

Lakini zaidi kwasababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiokuwa na changamoto. Na kuna muda changamoto ndio haswa zinatengeneza “character” zetu.
Kikubwa zaidi wakati wa changamoto tukumbuke kuwa wanyenyekevu, wenye kujishusha na kumuomba Mungu aendelee kutupa imani, hekima na busara ya kusubiri wakati wake. Tukumbuke Mungu hamtupi mja wake. Nawatakia Jumapili Njema. Nawapenda Sana. Ahsanteni ??”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.