Jux na Vanessa Waingia Matatani na Serikali Kwa Picha Yao Ya Kimahaba Stejini

Wanamuziki wa Bongo fleva Juma Khalid ‘Jux’ na mpenzi wake Vanessa mdee wamejikuta Kwenye upande mbaya wa sheria ya serikali baada ya kupiga picha ya kimahaba stejini.

Wikiendi iliyopita Jux na Vanessa walipiga shoo yao ya kwanza ya tour yao ya ‘In Love and Money’ mkoani Mwanza na kuonyeshana mahaba mazito stejini na hata kupigwa picha wakipeana mabusu.

download latest music    

Lakini sasa Global Publishers wanaripoti kuwa kitendo hiko kimewaingiza matatani kwani wamejikuta wakiuvaa moto wa serikali baada ya BASATA kuingilia kati.

Kwenye mahojiano na Gazeti hilo Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza alisema wao kama serikali picha hiyo imewachefua na hawajui ni shetani gani amewapata vijana hasa hao wanamuziki kwani kila kukicha wamekuwa wakionyesha vitendo visivyokuwa na maadili kwa jamii.

Sijui ni shetani gani amewaingia hawa vijana wanamuziki maana kila siku wanaonyesha vitu vya ajabu vizivyokuwa na maadili wanapokuwa jukwaani kwani hivi karibuni msanii Mbosso naye alifanya shoo na kuonyesha vitendo vilivyo kinyume kabisa na maadili, tukamuita na kumuonya na kumwagiza aombe msamaha kwa mashabiki na alifanya hivyo.

Sasa huyu Jux na Vanessa hata kama ni wapenzi hawakutakiwa kufanya hayo waliyoonyesha jukwaani kwani kama ni mahaba mnatakiwa muonyeshane mkiwa faragha na siyo hadharani kama walivyofanya tunawafanyia kazi ili kukomesha tabia hizo”.

Jux na Vanessa ni moja tu ya wasanii ambao wameshaonywa hivi karibuni kuhusu kufanya vitendo vya kimahaba stejini ambapo wengine ni Amber Lulu, Mbosso.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.