Kabula Amwagia Sifa Kiba Q Chillah Amuita Dhahabu

Muigizaji wa Bongo movie aliyewahi kutamba katika filamu ya Jumba la dhahabu Jini Kabula amefunguka na kuonyesha kuumizwa na Kitendo Cha Q Chief kutangaza kuacha mziki.

Mwezi uliopita msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Q Chillah aliweka wazi kuwa anataka kuachana na muziki baada ya kukata tamaa baada ya kushindwa kurudi kwenye chati kama zamani.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kabula ameamua kutoa ushauri juu ya maamuzi aliyoyafanya Q Chillah kuhusiana na kuachana na muziki.

Wee unaanzaje kumuacha mtu kama huyu apotee kizembe ifike mahali Taifa lipaze sauti kwa vijana nguvu kazi Chilla ni dhahabu ya Tanzania alipotangaza kuacha mziki roho ilipasuka nikasema No bado anauwezo mkubwa wa kuipeperusha bendera ya Taifa letu.

Wewe ni dhahabu kaka na dhahabu haiwezi ngaa bila kupita kwenye moto huwezi kuwa shujaa mpaka ukutane na mengi ya kukuumiza moyo na kukukatisha tamaa lazima udharauliwe ukataliwe na wakati mwingine kunenewa maneno ya uwongo ila ukiweza kutobowa hakuna anaweza kukushusha chini tena.

Sisi ni mashujaa wa Taifa ata tukiondoka leo tutaacha histolia ktk vizazi vijavyo acha ya zamani yaende simama ukainuliwe kaka…Watanzania tunakupenda tuko pamoja Maisha na mziki Go chilla”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.