Kajala Adaiwa Kumpindua Mke Wa Pfunk

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amezidi kukamata headlines kutokana na skendo yake yakurudiana na Baba watoto wake prodyuza mkongwe Paul Matthysen maarufu kama Pfunk Majani.

Kajala na Pfunk walikuwa kwenye mahusiano miaka kama kumi iliyopita ambapo walifanikiwa kuzaa pamoja mtoto mmoja lakini baadae waliachana na Pfunk kuwa na Mahusiano ya muda mrefu na mwanamke anayeitwa Samira ambaye pia amezaa naye mtoto mmoja na sasa mjamzito Tena.

download latest music    

Habari za chini ya kapeti za kimbea kabisa zinasema kuwa Kajala kampindua Samira kwa Pfunk hadi sasa inasemekana Samira amehama kwa Pfunk na amerudi kuishi nyumbani kwao kwa wazazi wake.

Habari hiyo imevujishwa na mtu wa karibu wa Samira ambaye ameliambia gazeti la Ijumaa Wikienda mambo haya:

Unajua P Funk kila alipokuwa akielezwa kuhusu Kajala alikuwa hanyooshi maelezo ingawa machoni alionesha kumpenda Kajala.

Mkewe ambaye kwa sasa ni mjamzito, ameishi kwenye kipindi kigumu sana. Anashindwa kumuelewa P Funk kwani watu kibao wanampigia na kumuambia wamemuona mumewe akiwa na Kajala”.

mtu huyo wa karibu na Samira alidai kuwa, mara kadhaa P Funk amekuwa akielezwa kuhusu …usaliti wake kwa Kajala lakini alikuwa akijitetea kwa kutumia kigezo cha kumlea mtoto aliyezaa na Kajala (Paula).

Yani Samira alikuwa akimbana P Funk lakini mara kadhaa P (P Funk) alikuwa anasema hakuna lolote zaidi ya yeye kwenda kumcheki mtoto hususan anapokuwa shuleni,” alisema mtu huyo. Akizungumzia picha zilizovuja, rafiki huyo wa Samira alisema shosti wake alivumilia zile picha za awali zilizomuonesha P Funk akiwa supermarket na Kajala lakini zilivyokuja kuvuja video wiki hii, ameona isiwe tabu afungashe virago vyake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.