Kajala afunguka kueleza kilichomfanya kujihusisha na utumiaji wa bangi

Kajala ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Wema Sepetu na pia muigizaji wa movie za bongo amefunguka kueleza sababu zilizofanya aanze kutumia dawa za kulevya Kama bangi na pombe.

Akizungumza na global publishers Kajala alisema kuwa marafiki wake wa hapo zamani ndio waliofanya aanze kuvuta bangi. Aliendelea kusema kuwa pia maisha yake ya wakati huo yalikuwa ya shida, na hii ilimfanya kutumia Madawa ili apunguze mawazo.

download latest music    

Unajua inafika mahali sisi kama vioo vya jamii inatupasa kuzungumza ukweli wa maisha yetu hasaa ya nyuma, ili kama ni watu kujifunza iwe hivyo, binafsi nimewahi kupitia maisha ambayo naweza kuyaita ya mpito, kipindi ambacho kila mtu hupitia katika harakati za ukuaji, kwamba nilijiingiza kwenye kampani za marafiki ambao ni watumiaji wa bangi.

Kulingana na Kajala anamshukuru mungu kwani hakupotelea kwenye maisha nayo. Hata hivyo alisema yeye hajawai kutumia cocaine, heroine wala kujidunga masindano

Hivyo, walinishawishi na kujikuta nikijiingiza kwenye ulevi huo, kidogo nipotee ila namshukuru sana Mungu kwani sikuwahi kuvuta madawa mengine kama cocaine, heroine sijui kujidunga masindano na mambo mengine ya kufanana na hayo, lakini ukweli kabisa huwa najuta sana kwa kuvuta bangi,” alisema Kajala na kuongeza; Ni muhimu wazazi kuwa makini na watoto katika kipindi cha kuingia kwenye utu uzima, kwa maana ya balehe ya kuvunja ungo, ndicho kipindi kibaya sana maishani kwa binadamu katika makuzi, vishawishi ni vingi sana.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua