Kajala Akana Tetesi Za Kuwa na Ujauzito Wa Pfunk

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja ‘Kay’ amefunguka na kukana tetesi zinazosikika Kwenye mitandao ya kijamii kuwa ana ujauzito wa PFunk.

Kajala na Pfunk walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka mingi iiyopita na baadae walijaliwa kupata mtoto mmoja pamoja anayeitwa Paula lakini siku za hivi karibuni imedaiwa wamerudiana.

download latest music    

Ingawa kajala ameshakataa kuwa hana uhusiano na Pfunk Tena zaidi ya kuwa marafiki kwa hivi sasa ili washirikiane kulea mtoto wao Paula inasemekana amerudisha majeshi kwa P.

Kwa habari zinazoshika kasi Kwenye mitandao ya kijamii kwa hivi sasa ni kuwa Kajala ameshika ujauzito wa Pfunk.

Kwenye mahojiano na   Over Ze Weekend, Kajala amedai kuwa amekuwa akiona  mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ishu hiyo, jambo ambalo anashindwa kuelewa limetokea wapi.

Jamani kwa nini watu wakimuona mtu amenawiri kidogo wanasema kuhusu mambo ya ujauzito? Mimi na P (Funk) mbona wanatung’an’ganiza sana? Wanashindwa kuelewa kabisa yule ni mzazi mwenzangu?” Alihoji Kajala akisisitiza kuwa hana kibendi“.

Miezi Michache iliyopita Kajala aliweka wazi kuwa alikuwa na ujauzito lakini kwa bahati mbaya ukaharibika ingawa hakuweka wazi nani hasa alikuwa muhusika.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.