Kajala Atoa Tamko Baada Ya Mtoto Wake Kufeli

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amefunguka na kutaka watu waache kumuongelea binti yake Paula kuwa amefeli kwani atahakikisha anafika chuo kikuu.

Wiki chache zilizopita Mtoto wa Kajal anayeitwa Paula alitengeneza headlines Baada ya matokeo yake ya kidato cha nne kutoka na kuonyesha kuwa amefeli mashabiki kwenye Mitandao ya kijamii walimjia juu na kuanza kumsema vibaya.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Kajala  ameamua kufunguka akishangazwa na watu kufuatilia na kutokwa povu na matokeo ya mwanaye, Paula.

Nafahamu kila kinachoendelea huko mtandaoni kuhusu matokeo ya Paula, niliamua kukaa kimya kwa kutojibizana na watu ili mwanangu abaki kuwa salama. Watu wanatakiwa kufahamu kuwa Paula ana wazazi wake, sio yatima hivyo kamwe hatakuwa mpweke.

Nashangazwa na inaumiza watu wanaacha kazi na kuanza kumrushia maneno makali mwanangu kwa lengo la kumkatisha tamaa, yaani kama ndio waliokuwa wakimlipia ada na huduma zingine. Watambue kuwa siwezi kumuacha mwanangu alie peke yake, nitakuwa naye kumtia moyo na kujipanga upya katika eleimu yake na atasoma hadi chuo kikuu“.

Lakini pia Kajala amesema kuwa matokeo yake kuwa mabaya hazina kabisa mahusiano na malezi anayolelewa nyumbani.

Unajua jambo linapotokea basi utayasikia mengi sana, Paula sio mtu wa starehe ya kwenda klabu sasa wamemuona wapi? Au ni malezi gani wanayataka nimlee mwanangu kwa sababu namlea kwenye maadili mema au hawataki niwe karibu na mwanangu ama kuwa na akaunti ya instagramu ni nongwa?.

Naomba wamuache mwanangu jamani, imetosha sasa na hao wanaotoa kauli za kejeli wenyewe wamesoma, narudia tena Paula atasoma hadi chuo kikuu na atakuja kuwashangaza“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.