Kajala-Siwezi Kuacha Kuongea na Baba Wa Mtoto Wangu Kisa Namuogopa Mke Wake

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi kuacha kuongea na Pfunk ambaye Baba wa mtoto wake Paula kwa sababu eti mke wake hapendi.

Wiki chache zilizopita Kumekuwa na Tetesi kuwa Kajala na Pfunk wamerudiana na Pfunk kumuacha mke wake ambaye amezaa naye mtoto mmoja na hivi sasa ana ujauzito mwingine.

download latest music    

Lakini pia wiki chache zilizopita mke wa Pfunk alilalamika na kusema Kajala anataka kumvunjia ndoa yake na hata kudaiwa alikuwa yuko tayari kufungasha virago vyake na kurudi kwa wazazi wake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Kajala amefungukia tetesi hizo na kusema anataka Samira ambaye ni mke wa Pfunk ajue kuwa yeye anaonana na Pfunk kwa ajili ya mtoto tu hana uhusiano naye mwingine Lakini pia hawezi kuacha kuonana kwa ajili ya mtoto wao.

Mimi sijamwambia aache ndoa yake kwa ajili yangu siwezi hata kumwambia hivyo! Ila ninachotaka kumwambia ni kuwa mimi na Pfunk ni lazima tuongee kwa ajili ya mtoto, Nilikaa miaka kama minne na P tunapishana hatusalimiani wala hatuongei lakini baadae nikaona tu ni ujinga tunamuumiza tu mtoto kwa nini tusisalimiane au P asiwe karibu na mtoto wake kisa ameoa? Wangapi wameoa na wanaangalia watoto wao”.

Lakini Kajala ameweka wazi kuwa ile video iliyisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha yeye na Pfunk wakibusiana mbele ya mtoto wao ilikuwa ni katika harakati tu za kumfurahisha mtoto wao.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.