Kaka wa Uwoya Afunguka Kuvunjika kwa Ndoa ya Dada Yake.

Babuu Uwoya kaka wa Irene Uwoya amesema familia yao kutomkubali Dogo Janja kuwa mume wa Irene Uwoya ndio chanzo cha ndoa hiyo kuvunjika
.
“Hakuna hata mmoja aliyependezewa na hilo suala, na hakuna hata mmoja aliyekuwepo kwenye harusi, sidhani kama ni ndoa, Dogo Janja alikuwa rafiki yangu, kasoma na wadogo zangu, hajawahi kuwa shemeji, mimi shemeji yangu namjua mmoja tu kashatangulia mbele za haki, anaitwa Ndikumana”, amesema Babuu alipoulizwa na East Africa Radio
.
Ikumbukwe miezi mingi iliyopita Mama Irene Uwoya akizungumza na gazeti moja serious hamtambui Dogo Janja Kama mkwe wake kwa madai hana adabu wala heshima ya kuwa mkwe wake

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.