Keisha Yupo Tayari kuchanganya Siasa na Muziki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka Tip Top connection Keisha amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kuwa kuna ugumu katika kuchanganya siasa na sanaa lakini yeye anaweza kumudu.

Keisha ambaye Miezi michache iliyopita alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) amesema hana Mpango was kuacha muziki.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Risasi Vibes, Keisha ambaye anatarajia kuachia video ya ngoma yake mpya ya Nioe alieleza kuwa, muziki na siasa ni kazi ambazo kwa upande fulani zinaen-dana kwa sababu unafa-nya kwa ajili ya watu amba-po kwen-ye muziki ni mashabiki na kwenye siasa ni wananchi ambao wanahitaji uwawakilishe na kutatua matatizo yao.

Ukiwa kwenye muziki unatakiwa kuwa na ubunifu, kujitoa na kujituma ndiyo vitu vya msingi ambavyo hata kwenye siasa vitu hivyo vinahitajika kwa kiasi kikubwa.

Kwa hiyo kuna ugumu fulani kufanya vitu hivi kwa pamoja, lakini ukiwa na moyo wa kufanya kama mimi, ni lazima utavimudu”.

Wasanii kadhaa walioingia Kwenye mambo ya siasa kama vile Profesa Jay na Sugu ambao wote ni wabunge wameonekana kuweka pembeni mambo ya muziki ingawa hawajatangaza kuacha au kustaafu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.