Kesi Ya Lulu Yaendelea Kuunguruma Leo, Hatma Yake Mikononi Mwa Baraza La Wazee Kesho

Kesi ya muigizaji wa bongo movie Lulu Michael ya kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake na mpenzi wake marehemu Steven Kanumba, imeendelea kusikilizwa leo mahakama kuu ambapo Askari Polisi Sargent Nengea amesoma maelezo aliyomwandikisha daktari wa Kanumba Josephine Mshumbisi.

Siku jana iliamriwa ya kuwa askari polisi aliyemuandikisha maelezo daktari wa Kanumba anatakiwa kufika mahakamani hapo kusoma maelezo hayo kutokana na kwamba Daktari Mshumbisi kuwepo nje ya nchi kwa sasa. Haya yafuatayo ni baadhi ya maelezo ambayo Askari polisi huyo alisoma;

download latest music    

Mmoja wa wateja wangu, marehemu Steven Kanumba kwa mara ya kwanza alikuja kwangu mwaka 2011 kwa ajili ya kutoa sumu mwilini. Marehemu alikuwa na matatizo ya damu, upungufu wa hewa kwenye ubongo, alikuwa anasikia maumivu katika ubongo na akili kuchoka sana”.

Polisi detective Sargeant Nengea alimalizia kusoma maelezo hayo yaliyotolewa na aliyekuwa daktari wa marehemu Steven Kanumba wakati wa uhai wake.

Baada ya kumaliza kusikiliza maelezo hayo ya upande wa daktari jaji aliamuru kuwa siku ya kesho tarehe 26 octoba, wazee wa baraza watakaa chini na kuamua na kujadili kama Lulu ana hatia ya hiyo kesi inayomkabili au hana.

Itambuliwe kuwa endapo lulu atakutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Kanumba na baraza hilo la wazee basi anaweza akahukumiwa kifungoo cha kuanzia miaka nane mpaka maisha jela.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.