Kesi ya Wema Sepetu Yahairishwa Tena

Kesi inayomkabili msanii wa bongo movies Wema Sepetu iliyokuwa imesikilizwa mara nyingine tena jana, imeharishwa tena mpka hapo February 26 mwaka huu.

Wema Sepetu ambae aliwasili jana viwanja vya mahakama ya Kisutu akionekeana asiye na wasiwasi akiingia kwa madoido katika mahakama hiyo huku  akiwa na wakili wake mpya Albert Msando baada ya yule aliyekuwa nae mwanzo kumbaga (Peter Kibatala) waliwasili pamoja na kuingia mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

download latest music    

Hata hivyo baada ya kesi hiyo kusoma, moja ya mashaidi aliewasilisha ushaidi wa mkojo wa Wema kutoka kwa mkemia mkuu huku wakili wa Wema akimuoji maswali yaliyomfanya shaidi huyo kuwa na kigugumizi muda mwingine.

Hata hiuvyo shaidi huyo amekiri kuwa wakati wa kufanya upekuzi katika nyumba ya Wema hawakufanya upekuzi katika chumba anacholala Wema zaidi ya chumba chake cha kulalia na chumba cha dada wa kazi ambapo walikutana na misokoto miwiwli ya bangi huku mmoja ukionekana kuwa ulishatumika.

Shaidi huyo ambae ni Inspecta wa polisi alipoulizwa kuhusu ni muda gani walitumia kukaa nje ya ofisi ya mkemi mkuu kusubiri sampuli ya mkojo wa wema alijibu kuwa hakumbuki muda  huo.

Kesi hiyo ya wWema inayomkabili kuhusu madawa ya kulevya itasoma tena February 26 na 27 mwaka huu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.