khadija Kopa Afunguka Skendo ya Kufumaniwa.

Mwanamuziki bora kabisa katika miondoko ya taarabu Khadija Kopa amfunguka na kutoa dukuduku lake kuwa katika vitu ambavyo aliwahi kuumizwa navyo sana katika maisha yake ni pale aliposingiziwa kuwa ameachwa na mwanaume wake kwa kupewa talaka kwa sababu alifumaniwa na mwanaume mwingine.

Akizungumza katika planet bongo ya EATV khadija ansema kuwa kipindi hicho waandishi wa habari walikuwa wakiandika mambo bila kuwa na ukwei wowote ili kupata habari lakini alimua sana kwa sababu haikuwa kweli hata kidogo.

download latest music    

skendo niliyokuwa nayo kubwa ni kipindi kile nilichotngazwa kuwa niliachwa kwa kupewa talak kisa tu nimefumaniwa, ila kiukweli sijawahi kufumaniwa ila watu tu waliamua kunizushia ili kusudi kwao yaende na kipindi hicho kulikuwa hakuna hata mitandao ya kijamii.

Mimi huwa istafuti kiki ila kiki zinakuja znyewe, nilikuwa sipiti siku bila kuweka front page za magazeti , waandishi walikuwa wanafanya tu vile walikuwa wanataka kuandika.

Hata hivyo khadija kopa anasema kuwa kitu kikubwa kilichomfanya mpaka sasa aweze kudumu katika game ni kwa sababu amekuwa akibadilika kulingana na mazingira ya muziki.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.