khassim Mganga Apanga Kutoa Ngoma Mpya Kila Siku

Msanii khassim Mganga amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba amekuwa akitoa ngoma kwa kusua sua  lakini sasa hivi ameona kuwa atakuwa akitoa ngoma mpya kila siku kwa sababu mashabiki wanataka burudani mpya kila siku.

Akiongea katika clouds media, khassim anasema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akitunga ngoma mpya kila siku lakini hakuwahi kuzitoa kwa muda mrefu, hivyo sasa ameona kuwa atakuwa akitoa ngoma mpya kila siku mpka zilizopo store ziiishe zote.

download latest music    

Hakuna haja ya kuweka ngoma ndani,ni mawe juu ya mawekila mwezi nitaanza kutoa ngoma mpya kwa sababu kila siku huwa narekodi, kwa sababu ngoma tunawaandikia mashabiki basi  sioni haja ya kuziweka ndani.

khassim mganga ni moja ya wasanii wakongwe waliowahi kufanya vizuri na wanaoendelea kufanya vizuri kila siku na amekuwa akifurahia ujio wa wasanii wapya ambao wamekuwa wakileta chachu ya muziki Tanzania.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.