Kibenteni Kilinigeuza Mimi ‘ATM’ Yake – Nisha

Muigizaji wa Bongo movie ambaye hivi karibuni amegeukia tasnia ya Bongo fleva na kuachia wimbo wake unaojulikana kama ‘Bachela’ amefunguka jinsi kibenteni chake kilivyokuwa kinamchuna.

Nisha amefunguka na kuelezea jinsi alivyowahi kuteswa na penzi la kijana mwenye umri mdogo kuliko yeye kwani ilibidi yeye ndio awe anampa huduma zote kijana yule.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nisha amesema kuwa wakati akiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kibenteni huyo ambaye hakutaka kumtaja jina alikuwa akimnunulia kila kitu na kumpa fedha na kumuhudumia kama mtoto wake lakini baadaye alikuja kushtuka kuwa anachunwa na kua­mua kuachana naye.

Nimejifunza sana na nime­koma kuwa na uhusiano na mwanaume ninayemzidi umri na kipato maana nilijikuta nime­ingia kwenye uhusiano huo bila kujua kwamba kibenteni huyo ni tege­mezi ambaye alinifanya kama mashine yake ya ATM na kuniko­moa kuja kushtuka ameshanikwan­gua vya kutosha”.

Nisha ingawa amekiri kuwa mara ya kwanza wakati anaanza mapenzi na kijana huyo hakujua kuwa ni mdogo lakini baada alimpenda na kuendelea naye jambo ambalo anajutia kupita kiasi.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.