Kifo Cha Kanumba Kilisababishwa Na Mengi

Ikiwa kesi ya kuuawa kwake bila kukusudia bado  ikiendelea na kuonekana kukaribia  kufikia ukingoni mahakamani, shahidi ambae alikuwa akisubiriwa kutoa ushahidi wake ili kupisha maamuzi kukamilika  pia alikuwa ni daktari wa marehemu Steven Kanumba , Dk. Josephine Mushumbusi amewakilisha ushaidi wake mahakamani uliosomwa na askari .Ushahidi huo ulioandikwa na daktari huyo miaka iliyopita na daktari huyo ukielezea hali aliyokuwa nayo marehemu kabla ya kifo chake umepokelewa mahakamani.

Ushahidi huo ambao mara ya kwanza  ulikataliwa kupokelewa na mahakama mpaka pale shahidi huyo awepo mahakamani au polisi alikuwepo kipindi ushahidi unaandikwa ndie aweze kusoma ushahidi huo , umepeokewa mahakamani tarehe 25 oktoba  huku maelezo yakisema kuwa marehemu alikuwa na magonjwa mengine na  alikuwa akienda cliniki kutibiwa mara kwa mara.

download latest music    

Katika ushahidi huo,wenye maelezo ya daktari huyo  ulieleza kuwa daktari Josephine Mushumbuzi alikuwa akimfahamu marehemu Steven Kanumba kama mgonjwa wake aliekuwa akienda katika ofisi zake zilizopo jengo la mawasiliano kufanya matitabu na vipimo “Steven alikuwa  na matatizo ya sumu mwilini, na alikuwa anakuja katika  kituo cha clinic yangu  ambapo alikuwa  akifanya vipimo vya mwili  vya mwili mzima na alikutwa na tatizo la mafuta mwilini (cholestrol), tatizo la moyo, na upungufu wa hewa ya Oksijeni  kwenye ubongo  ambayo ilikuwa ikimsababisha maumivu makali mara kwa mara.” ulieleza ushahidi huo.

Hata hivyo daktari huyo alisema kuw mara ya mwisho kufanyiwa vipimo hivyo alishindwa kumfanyia baadhi ya matibabu na walipanga kukutana clinic hapo siku nyingine kwa ajili ya matibabu  zaidi lakini hawakukutana tena mpaka mauti yalipomkuta.

Hata hivyo kesi hiyo imeshafungwa upande wa kusikilizwa kwa mashahidi ambapo kitu kinachosubiri sasa  ni baraza la wazee kuangaalia ushahidi wa pande zote mbili na kutoa maamuzi ya mwisho.

Elizabeth Lulu Michael na  Steven Kanumba walikuwa katika mahusiano ya mapenzi kwa muda na mahusiano yao yalikuwa ya siri,marehemu alifariki baada ya kudondoka chini nyumbani kwake Sinza Vatican alipokuwepo na mpenzi wake huyo  ,ambapo walikuwa na ugomvi.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.