Kifo Cha Mtoto wa Muna Chagubikwa na Utata Mzito

Siku mbili zilizopita mtoto wa Muigizaji wa Bongo movie na mdau wa muziki wa Bongo fleva Muna Love, Patrick alifariki dunia kutokana na ugonjwa alioumwa kwa miaka miwili.

Lakini tangu Kifo hiko kitokee kumetokea na utata mkubwa katika msiba wa mtoto huyo kwani mpaka sasa misiba imewekwa sehemu mbili kwani haijajulikana Baba wa mtoto ni nani.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Mwanaume anayeitwa Peter ameibuka na kudai yeye ndiye Baba wa mtoto na kusema yeye ndio mume halali wa Muna Kwenye ndoa waliyofunga kanisani mwaka 2010.

Peter ambaye anaishi Mwananyamala ameweka msiba kwake na kudai yeye ndiye aliyemlea Patrick kuanzia amazaliwa na yeye ndiye amemsomesha mtoto mpaka anafikwa na mauti na juzi tu yeye ndio ametuma pesa ya dawa hospitali Nairobi.

Lakini siku zote Baba wa mtoto anayejulikana ni Casto Dickson ambaye na yeye amesisitiza kuwa yeye ndio baba halali wa mtoto baby kudai yeye ndio aliyemlea Patrick tangu mdogo.

Mpaka sasa kuna utata kwa sababu misiba iko sehemu mbili tofauti yaani nyumbani kwa Muna Mbezi Beach na nyumbani kwa Peter Mwananyamala.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.