Kifungo cha Lulu Chabakiza Siku 40.

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael ’Lulu’, amebakiza siku 40 kumaliza kifungo chake huku akielezwa kuwa mtiifu kipindi chote.

Lulu alikuwa akitumikia kifungo cha miaka miwili jela, baada ya Novemba 13, mwaka jana kuhukumiwa na mahakama kuu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa gwiji wa filamu, Steven Kanumba.

download latest music    

Hata hivyo, Aprili 26 mwaka huu, msanii huyo aliye kwenye orodha ya wadada wanaojua kuvaa  hapa Bongo alibadilishiwa adhabu hiyo na kuwa ya kifungo cha nje.Kutokana na hilo, alipangiwa kazi ya kufanya usafi katika Wizara ya Mambo ya Ndani iliyopo maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam aliyoianza tangu Machi 14 mwaka huu.

Katika siku za mwanzo gazeti la Mwananchi lilipata picha akiwa ameanza kutumikia kifungo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa Probesheni na Huduma za Jamii, Charles Nsanze, amesema katika kipindi chote hicho Lulu amekuwa akitekeleza majukumu yake bila kukosa. “Amekuwa mmoja wa wafungwa wenye nidhamu ya hali ya juu na hakuna siku aliyokosa kuja na kufanya kazi kama alivyopangiwa,” amesema Nsanze alipoulizwa kuhusu utumikiaji adhabu wa msanii huo ulipofikia hadi sasa.

Kifungo cha Lulu kilipaswa kuisha Machi mwakani endapo asingebailishiwa adhabu ya kifungo gerezani na kuwa kifungo cha nje baada ya kupata msamaha wa Rais.Magereza ilifafanua kwamba ina utaratibu wa kutoa msamaha wa theluthi moja ya kifungo na msanii huyo alinufaika baada ya kuonyesha tabia njema.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.