Kimnana Atuliza Moyo Wake Kwa Otile Brown

Video vixen na aliyekuwa Mpenzi wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Kimnana anasemekana kuutuliza moyo Wake Kwa msanii kutoka Kenya Otile Brown.

download latest music    

Kimnana alijizolea umaarufu Baada ya kuanzisha uhusiano na Diamond miezi michache iliyopita lakini mahusiano hayo yaliingia shubiri Baada ya Diamond kumtosa Wiki chache zilizopita na kuanzisha mahusiano na mrembo kutoka Kenya Tanasha.

Baada ya kumalizana na Diamond, Kimnana amesonga mbele kwani hivi sasa anadaiwa kuwa kwenye mahusiano na Otile ambaye ni Ex boyfriend wa Socialite Vera Sidika kutoka Kenya.

Wawili hao walionekana pamoja nchini Kenya Wiki iliyopita na kuzua maneno kutokana na ukaribu wao  waliouonyesha kutokana na kukumbatiana na maneno mengine.

Otile Brown hajaweka wazi Kama Wapo kwenye mahusiano lakini amemuandikia ujumbe wa shukrani mrembo huyo kupitia ukurasa wake Wake wa Instagram:

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.