Kisa Cha LavaLava Kuimba ‘Tuachane’ Hiki Hapa

Msanii aneafanya vizuri kimuziki kutoka katika kundi la wasanii wenye vipaji nchini  Wcb-Wasafi ambae ngoma yake ya kwanza kumtambulisha ilikuwa ni ile ya Tuachane ameelezea kiundani sababu ya yeye kuimba wimbo huo .Lavalava ambae anasema kuwa wimbo huo ni moja ya vitu vilivyomtokea katika maisha hivyo aliimba wimbo huo akiwa na hisia za maumivu kutokana na kile kilichomkuta siku za karibuni kabla ya kutoawimbo huo.

Lavalava ambae anasema kuwa alikuwa akiishi nyumba moja na mwanamke ambae yeye alikuwa akimchukulia kama wa kwake kumbe alikuwa na mwanaume mwingine na hata ile nyumba waliokuwa wanakaa ambayo alihisi kuwa analipa mwanamke huyo  kumbe  alikuwa akilipiwa  na mwanaume mwenzie.

download latest music    

Mwezi mmoja kabla sijaachia ngoma ya tuachane nilikuwa na mpenzi wangu ambae tulikuwa  tumepanga na tunakaa pamoja, tulikuwa tumepanga mipango mingi ya maisha kwamba kuan siku nitafika tutafanikiwa  na nitaweza kumuhudumia , afu na yeye akawa ananihitikia tu fresh,kumbe bhana hata pale tulipokuwa tunakaaa kuna mwana alikuwa amempangishia.-Alifunguka mwanamuziki huyo kutoka kundi la Wasafi

Na mimi nikawa ninakaa hapo najiachia, mchizi siku hiyo akarudi akanikuta yaani nilihisi kama nataka kufa  kufa hivi, akaniambia mi ndo baba mwenye nyumba nimerudi hapa kwangu.-Aliendelea kusema Lavalava.

Akiendelea kuongea na Radio Free Lavalava nasema kuwa baada ya hapoa aliwaacha wakaendelea kubembelezana yeye akaamua kondoka ndipo  alipoamua kwenda kutoa wimbo wa Tuachane.

Vijana wengi wa kiume wamekuwa wakikaa na wapenzi wao  wa kike bila kujua kuwa  mwanamke anaeishi nae anakuwa yupo na mahusiano na mwanaume mwingine na hata matunzo anayopata yanatoka kwa mwanaume mwingine, kwa upande wa vijana ambao wengi wanapenda kulelewa  wamekuwa wakiumizwa sana na mambo kama hayo ingawa kwa Lavalava anasema kuwa yeye aliamini kuwa ni mwanamke atakae panga nae maisha kwa ajili ya baadae.

kwa vijana wengi , inabidi ifike sehemu watu waingie katika mahusiano huku akiwa ameshafanya uchunguzi na kumjua vyema mtua aneingia nae katika mahusiano.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.