Kisa Esma , Mama Diamond Asota Polisi Masaa 6

Wikiend iliyopita mama mzazi wa Diamond Platinumz amejikuta akiingia matatani na kushinda kituo cha polisi baada ya mtoto wake wa kike esma platinumz kukamatwa na polisi baada ya mamlaka inayohusika na kukagua madawa vyakula na vipodozi kumkata mwanadada huyo.

Esma alitiwa mbaloni na polisi baada ya maafisa ya TFDA kugundua kuwa anauza vipodozi vyenye kemikali na kwamba kuna vingine haviruhusiwi kabisa kuuzwa katika saluni yake iliyopo sinza afrika sana jijini dar.

download latest music    

Taarifa zilielezea kuwa esma alikamatwa baada ya maafisa hao kupita katika mduka mbalimbali wakifanya msako wa kuwakamata watu wanoendelea kuuza vipodozi vyenye kemikali ndio mama yake alipoambata na Petit Man ambae ni mume wa Esma mpaka kituoni hapo kwa ajili ya kumnasua mikononi mwa polisi.

Mama diamond ambae alikuwa akionekana kulumbana na polisi ili mwane kuachiwa aliambiwa  na polisi kuwa sio jukumu lao kumtoa Esma mpaka watakapopata amri kutoka kwa maafisa wa TFDA kwanza ndio waweze kumuachia.

Hata hivyo mpka siku ya jumamosi mchana mwanadada huyo bado alikuwa akishikiliwa na polisi kityuoni hapo na maswala mengine ya kisheria yakiendelea.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.