Kisa Kikuku Vanessa Ampiga Mkwara Jux

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ameweka wazi kuwa amemchimba mkwara mzito mpenzi wake Jux kuhusiana na kuvaa kikuku.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Vanessa amefunguka kuwa uvaaji wa vikuku sio utamaduni wa wanaume wa Kitanzania hivyo hawezi pendezwa na utamaduni huo kwa madai umamshushia heshima mwanaume.

download latest music    

Kusema kweli Jux hawezi kuvaa kikuku  Sidhani kama inaendana na tamaduni zetu. Vikuku ni kwaajili ya wasichana, sipendi japo naona kuna watu wengi wanavaa”.

Vanessa aliongeza kuwa;

Kiukweli kuna msanii wa Marekani anampenda Jux anaitwa Fabulous, na yeye nahisi anavaa kikuku, nikasema nini hiki, nikamwambia ole wako na wewe uvae”.

Siku chache zilizopita Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz alizua gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa amevaa kikuku Kwenye mguu jambo ambalo watu wengi halikuwavutia.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.