Kisa Mpira, Ray Amtolea Povu Haji Manara

Msanii wa bongo movies Ray Kigosi amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba katika mpira kuna mechi unaweza kushinda na zingine ukashindwa lakini kwa upande wa Hajis Manara anatakiwa kuacha kuwadanganywa mashabiki kuwa kila mechi watashinda na mwisho wa siku wanafeli katika mechi hizo.

Ray anasema kuwa Hajis Manara muda wote amekuwa akiwapa moyo mashabiki wakati hakuna kitu cha maana wanachofanya wachezaji wakiwa uwanjani , hivyo basi ni bora kila wanapotakiwa kuongea na mashabiki wao wawe wanaongea ukweli kuhusu simba na sio kuwadanganya mashabiki.

download latest music    

Hata hivyo pamoja na kuwa msanii wa maigizo , Ray amekuwa moja kati yawasanii wanaoshabikia mpira na hata kuingia katika mabishano ya mpira, watu wengine ni kama Jokate, JB, Wema Sepetu na Mbonnie Masimba.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.