Kocha wa Coastal Union Awatoa Wasiwasi Mashabi kiKuhusu Kutokuonekana kwa Alikiba Uwanjani

Msanii Alikiba ambae hivi karibuni amekuwa haonekani kabisa uwanjani  katika ligi inayoendelea kwa sasa katika mpira wa miguu  alianza kuwatia mashabiki wake hofu kwamba kwanini amekuwa haonekani akicheza au labda kiwango kimeshuka.

Baada ya baadhi ya mashabiki kuhoji, kocha mkuu wa timu hiyo ametoa taarifa rasmi kuhusu swala hilo na kusema kuwa katika ligi hii kuna mechi zaidi ya 30 na zote zinatakiwa kuchezwa hivyo Alikiba kutoonekana katika mechi hizi haimaanishi kuwa basi ametoka katika mchezo bali ataanza kuonekana mechi zijazo.

download latest music    

Alikiba ni mchezaji wa coastal union, na amesajiliwa  kwa uwezo wake na kuna mechi zaidi ya 30 za kucheza  kwaio nina uhakika kuwa muda ukifika Alikiba atacheza tu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.