Koletha Afunguka Jinsi Mtoto Wake Alivyomliza

Msanii mkongwe wa filamu za Bongo movie Coletha Raymond maarufu kama Koletha amefunguka na kuweka wazi kipindi kigumu alichopitia alipokuwa nchini China.

Koletha ameeleza kuwa kuwa alikesha akilia alipokuwa Beijing nchini China wakati akifanya kazi huko kisa kikiwa ni kumkumbuka mtoto wake aliyemuacha Tanzania.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Koleta ambaye alipotea kidogo kwenye kuigiza, alisema alienda Beijing kwa ajili ya kufanya kazi ya kuingiza Sauti za Kiswahili kwenye tamthiliya za Kichina, lakini alimuacha mtoto wake akiwa na mwaka mmoja tu kitendo kilichosababisha kila akimkumbuka anaji-fungia na kulia.

Jamani nilivyokuwa kule kwa mara ya kwanza ndio nimejua mtoto anauma maana kila nilipokuwa natoka kazini nilikuwa na¬jifungia ndani, nalia mpaka wenzangu wanakuja kunibembe¬leza na kunipa moyo, nilijitahidi mpaka nikazoea ila kwa shida sana kwa sababu tu ilikuwa ni kazi lakini mtoto anauma jamani“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.