Kuchora Tattoo ni Ushamba:-Whozu

Msanii chipukizi WHOZU anatamba na nyimbo ya Follow un follow amediss Show Off zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii hususani instagram kuhusu wasanii na mastaa mbalimbali kuchora tattoo zanye majina ya wapenzi wao.

Akizungumza na wasafi Tv Whozu amesema huo ni ushamba na show off za zamani mtu mwenye mapenzi ya kweli awezi kufanya vitu vya hadharani na kudanganyana tu.

download latest music    

“Hata siamini katika kuchora tatoo ndo mapenzi sifikiliagi kabisa kwakuwa njia ya tatoo ni ya zamani sana hata kama unampenda mtu kukubaliana hali ya maisha ndo mapenzi ya kweli na sio kucholana mambo haya ni kuiga tu siku mkizinguana pale kwenye tatoo unachora chura na wanaofanya hivo mara nyingi usiku ni vipigo tu kuchorana tatoo ni kudanganyana tu na show off za kijinga” alisema Whozu

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mtangazaji wa clouds Fm Casto Dickson aliamua kuchora tatoo ya jina la mpenzi wake ambaye ni Tunda kwenye mkono wake na kuibua mzozo mkubwa kwenye mtandao wa kijamii ila si yeye ni wa kwanza kufanya hivo bali wengi wamewahi kufanya hivyo kama msanii dogo janja alichora Tatoo ya Mkewe Irene Uwoya, hata nuh mziwanda alipokuwa na shilole aliwahi kuchora tatoo ya mpenzi wake huyo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.