Kufungia Nyimbo Kwawaingiza Matatani BASATA.

Baraza la sanaa Tanzania limefunguka na kusema kuwa kitendo cha wao kuamua kuwawajibisha wasanii kwa kuwafungia nyimbo ambazo zimekuwa hazina maadili limekuwa baya baada ya wao kuingia matatani kwa kipindi kirefu sasa tangu wameanza zoezi hilo.

Mh Godfrey Muingereza anasema kuwa kwa mwaka 2019 wanahaidi kufanya vizuri zaidi hasa katika kuwaweka wasanii katika mstari ulionyooka kwa kufuata katiba na sheria za baraza hilo ingawa kumekuwa na cgangamoto mablimbali .

download latest music    

Kiongozi huyo anasema kuwa wamekuwa na wakatI mgumu sana hasa wanapoanza kutishiwa maisha, kukatwa mapanga na hata kumwagiwa tindikali wakati nia yao ni kuwawea wasanii katika mstari sawa ili kulinda na kukuza muziki na tamaduni pia.

Ikumbukwe kuwa , BASATA wamekuwa mstari wa mbele kukemea kitu chochote kinachohusu sanaa mbacho kinaweza kukiuka maadili na kupotosha jamii kupitia sanaa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.