Kumfungia Nyimbo ni Kumuua Msanii:-Jux

Msanii wa bongo fleva juma jux amefunguka na kusema kuwa kitendo cha BASATA kufungia nyimbo za wasanii sio kitu kizuri na kimekuwa kikiwaathiri sana wasaniiwengine hata kama BASATA wanakuwa hawaobi nikwakiasi gani wanawaumiza wasanii.

jux ambae pia wimbo wake wa uzuri wako ulifungiwa , anasema uwa wimbo wake umefungiwa miaka kama mitano iliyopita hivyo alikuwa ameshafuta machozi na kidonda kimepona lakini walipoutoa tena katika lish]t mpya imekuwa kama wanatonesha kidonda na kuonyesha kuwa wanatilia mkazo maamuzi yao.

download latest music    

Wimbo wangu ulifungiwa miaka kama mitano iliyopita,nilijaribu kufatilia lakini hakuna feedback yoyte niliyopata ,na kisa ni maadili hayohayo.lakini pia kuitoa tena sasa hivi kunaonyesha kuwa wanataka kutilia mkazo lakini wanatonesha kidonda kilichopona.

Kuhusu kukosewa kwa jina lake katika list hiyo ya majina na nyimbo zilizofungiwa , jux anasema kuwa hajui kwa nini walikosea jinalake lakini anajua kuwa serikali inamtambua.

Kuhusu jina langu kukosewa hapo hata sijui ingawa kuna baadhi ya watuwalisema kuwa inawezekana sitambuliki na BASATA  lakini  sidhani kwa sababu nilishawahi kushinda hata tuzo.sasa inakuwaje wanakosea jina langu.

Maoni ya mwisho ya jux kwa BASATA ni kwamba kama wanaona kuwa kuna kitu cha kuzngumza na msanii ni bora kufanya hivyo kabla ya kufikia uamuzi wa kufungia nyimbo zao.

Kufungiwa nyimbo sio jambo zuri kabisa , hii ni kama kumuu msanii tu .na hii nadhani BASATA wanatakiwa wakae na wasanii kujua tatizo lao kwa sababu huu ndo muda ambao biashara ya muziki ndio inaanza kuamka.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.