Kuna nini Kati ya Vanessa Mdee na baby Madaha?

Msanii wa Bongo baby Madaha amedai kuwa kwenye industry ya bongo hakuna waimbaji wa kike ambao wanatalanta ya kuwafanya kuwania Tuzo za kimataifa.

Akizungumza na watangazaji wa Sibuka FM katika kipindi cha 180 Power, Byno na Joco, baby Madaha aliskika akimgusa Vanessa Mdee kwa kusema kuwa kunawaimbaji wa kike ambao hutajwa kuwania tuzo mbalimbali ilhali hawashindi hata moja.

download latest music    

Hata hivyo maneno yake yalionekana kumlenga vanessa ambaye nimsanii wa kike kutoka Tanzania ambaye amewania tuzo kadhaa. Baby Madaha alisema,

“Tunapeleka watu kuwania tuzo wengine hawana vigezo vya hizo tuzo, especially nazungumzia kwa madada kuna dada mmoja yaani kila tuzo anaendaga lakini ashindi kutokana na nini hana qualification za hizo tuzo,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua