Kupunguza Mwili Kunanipa Madili Mengi :-Gigy Money

 

Msanii wa bongo fleva Gigy Money, Amefunguka kuwa yeye kupungua kwake kunampa faida sana katika kupata madili na kuwa mwepesi kwenye show zake.

download latest music    

Akizungumza na eatv.tv Gigy Money amesema kama angeendelea kuwa mnene basi kwenye kutumbuiza jukwaani asingekuwa mwepesi kama alivyo sasa hivi kwa hiyo hapendi kuwa mnene tena.

Gigy Money amesema unene sio mzuri kwa kile alichodai kwamba mtu akiwa mnene anakuwa na mwili usiokuwa na mvuto sana kama ukiwa mwembamba, na pia raha ya kuwa mwembamba unakuwa shapu shapu kwa kila kitu ambacho unakuwa unaitaji kufanya kwa wakati.

Kwanza mimi nafurahia kuwa mwembamba kuliko nilivyokuwa zamani, moja ukiwa mwembamba kwenye ‘show’ unafanya utakavyo tofauti na ukiwa mnene kingine ona mtu kama Vanessa akiwa nafanya ‘show’ hadi una-enjoy kwa hiyo kuwa ki-model pia unapata matangazo mengi” ,amesema Gigy Money.

Ameongeza kwa kusema anapokuwa kwenye jukwaa ana kuwa huru kufanya chochote kuliko zamani alivyokuwa kwa hiyo hapendi kurudi katika hari ile ya zamani ya unene.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.