Kutokuwa na Mtoto Hakujawahi Kunifanya Nikose Amani :-JB

Mkongwe wa nchini, Jacob Steven maarufu kama JB amewafungukia wale wote wanaodhani kuwa swala la kukosa mtoto kwenye ndoa linamfanya akose furaha maishani mwake.Wat wengi wamekuwa wakimshangaa msanii huyo kutoka na kuwa n afuraha na wala hakuwahi kulalamika kuhusu swala hilo.

Kwenye moja ya mahojioni aliyofanya Jb amefunguka na kusema “Ndio nakaribia miaka 50 na sina mtoto, sijabahatika kupata mtoto kwenye ndoa yangu, lakini kutokuwa na watoto maishani mwangu haijawahi kunifanya nikose amani au nimchukie mke wangu, Nampenda sana mke wangu na ipo siku naamini Mungu atatupatia mtoto au tusipopata kabisa pia tutamshukuru lakini sitaweza kukufuru.

download latest music    

Jb ameyasema hayo kukanusha imani ya baadhi ya watu wengi wanaoamini furaha ya ndoa ni mtoto na endapo atakosekana kwenye ndoa basi upendo kwa mwanaume utashuka kwa mkewe.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.