Kwani Diamond ni Nani:-Chemical

Mwanamuziki wa hip-hop nchini Chemical ameshangazwa sana na mafanikio ya Diamond platinumz huku wasanii wengine wakibaki kumsifia kwa mafanikio yake bila kuwa na nguvu na jithada za kumfikia msanii mwenzao.

Chemical anahoji kuwa kwani Diamond ni nani mpaka anafikia kuwa na mafanikio makubwa kuliko msanii yoyote nchini ilihali wakati anaanza muziki aliwakuta wasanii wengine wengi wenye jina lakini amewapita katika mafanikio.

download latest music    

chemical aliandika “Diamond ni nani kwani , hivi kweli wasanii woote tuliopo tanzania tumeshindwa kufikia usta na mafanikio ya kaka chibu? hata wale kaka zetu na dada zetu waliotangulia wameshindwa  mpaka Tanzania nzima msanii maarufu na mwenye mafanikio makubwa yanayoonekana  ni Diamond  tu , kwani tunakwamba vipi.”

Pengine kuhoji kwa chemical hakumaanishi kuwa anamuonea wivu msanii huyo mkubwa pengine anaona ina kuwa ngumu kwa wasanii wengne kutoboza na kufanya makubwa anayoyafanya Diamond.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.