Lava Lava afunguka kuhusu bosi wake wa Wasafi Records

Lava Lava ndiye msanii mpya kwenye label ya Wasafi Records na baada ya kuachia wimbo wake mpya bora Tuachane msanii huyo ameonyesha kuwa anatalanta ambayo itampeleka mbali.

Hata hivyo hivi karibuni akizungumza na Mzazi Willy M Tuva kwenye kipindi cha Radio Citizen, Lava Lava alisema kuwa ilimchukua muda wa mwaka mmoja kukutana na Diamond Platnumz macho kwa macho.

download latest music    

Kulingana na Lava Lava hii ilikuwa kama mtihani kwake kwa sababu kuna wakati akate tamaa. Alimwambia Willy

“Ilikuwa inanivunja moyo sana, kwamba sasa itakuwaje na ndoto zangu ni kumuona Diamond kwa sababu ni kioo chetu mtaani tunamuangalia nikaona kama itakuwa hanifuatilii kumbe yeye anafuatilia stori zangu sema ni katika kuniona kama nina moyo na uvumilivu,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua