Lava Lava awatetea wasanii wa Wasafi records baada ya wengi kudai kuwa wanamuiga Diamond Platnumz

Lava Lava ambaye ni msanii mpya wa Wasafi records kwa hivi sasa anatamba kwa wimbo wake mpya ‘bora tuachane’ ambao umempa mashabiki wengi kwa muda wa wiki moja.

Baada ya kuingia Wasafi msanii huyu amepata interview kadhaa kwa redio na hivi karibuni tunatarajia kumuona kwenye televisheni.

download latest music    
Lava Lava
Lava Lava

Hata hivyo kama wasanii wenzake, msanii huyu ameweza kupata changamoto ambazo zinaweza kuiletea career yake shida. Hivi karibuni akizungumza kwenye interview na Bongo 5 msanii huyu alikana kuwa hakuna msanii yoyote kutoka Wasafi Records anayemuiga Diamond Platnumz. Kulingana na yeye kila mtu ananjia tofauti ya kuimba na iwapo saa zingine wengi wanaona kuwa wanaimba kama mkubwa wao…hii sio ukweli.

Alisema,

“Naona watu wanazungumza lakini watu wawe na masikio ya kusikiliza kitu. Sio watu wote wanaweza kufanana ya Diamond japokuwa kuna vitu tunaweza kufanana kwa sababu ni watu ambao tunakaa pamoja kwa muda mrefu. Pia watu wakiwa wanaishi muda mrefu pamoja huwa wanafanana, kwa hiyo kuna muda mkikaa pamoja kuna vitu mnaanza kushare lakini ukichunguza ndani yake kila mtu ana kitu chake,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua