Linah Akiri Kuvutiwa na Mastaa Wa Mbele

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Linah Sanga aka Ndege  Mnana amefunguka na kuweka wazi kuwa anavutuwa sana na maisha ya mastaa wa mbele hasa Cardi B na Beyoncé.

Linah amesema anavutuwa sana na wasanii hao kwani ameona kuwa pamoja na kwamba wamepata watoto na kuwa wamama lakini wameendelea na maisha ya sanaa kama kawaida.

download latest music    
Beyoncé na Cardi B

Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Linah ambaye tayari ni mama wa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris amesema kitu hicho kinaendelea kumpa morari ya kufanya Muziki.

Beyonce alijifungua mtoto mmoja na mara ya pili alijifungua watoto mapacha lakini bado akipanda kwenye jukwaa unaweza kusema amepanda mtu ambaye hana mtoto hata mmoja. Ukimwangalia tena Cardi B sasa ana ujauzito mkubwa tu ambao anakaribia kujifungua lakini ebu angalia perfomance yake na the way anavyokwenda.

Kinachonifurahisha ni kwamba hata ile dhana yetu kwamba ukianza tu kuwa na familia umeharibu kwa sababu huwezi kusema wewe ni mwanamuziki usizae, inabidi uwe na familiaa yako na uwe na mume wako lakini uwendelee na kazi yako”.

Wasanii wengi wa kike Tanzania wamekuwa wakikumbana na kasumba ya kutakiwa kuacha kufanya Muziki mara tu wanapozaa na wengine huachana na Muziki pale wanapoolewa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.