Linah Awajia Juu Wanaomponda Mtoto Wake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Linah Sanga ameibuka na kuwajia  juu watu ambao wamekuwa wakimponda binti yake.

Siku chache zilizopita Linah alituhumiwa kwa kuedit  picha za mtoto Wake Paris Tracey mwenye umri wa mwaka mmoja kiasi cha kubadilisha rangi yake na kuwa mweupe kabisa.

download latest music    

Linah ambaye ni mama wa mtoto huyo mmoja, amefunguka ikiwa ni siku chache baada ya picha ya mwanawe kusambaa mitandaoni ikimwonyesha akiwa tofauti na jinsi mama yake anavyomuweka.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba Jumatano, Linah, alisema amekua akitumia uhuru binafsi kuishi na mtoto wake hivyo hapendi jinsi watu wanavyomtuhumu na kutaka kumpangia maisha ya mwanawe.

Ifike mahali kila mtu afanye yale maisha anayoona yanamfaa, mambo ya kupangiana maisha si sawa kwa kizazi hiki, kuna watu wanalalamika na mposti mwanangu tofauti na alivyo wajue nafanya hivi kwa mapenzi yangu na si yao”.

Linah amekua akimwonyesha mwanawe lakini watu wengi wamedai mwanadada huyo amekua akimbadilisha zaidi mtoto huyo rangi ya mwili wake na kuonekana mweupe tofauti na alivyo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.