Linex Ajutia kutoonana na Godzilla Kabla ya kifo chake.

Msanii Linex Sunday Mjeda amefunguka na kuonyesha jinsia alivyoguswa na msiba wa msanii Godzilla hasa baada ya kujutia uamuzi wake wa kutotaka kuonana nae kabla ya kifo chache.

Linex anasema kuwa , msanii mwenzake huyo alitaka kuonana siku kama tatu kabla ya kifo chake lakini alimuomba wakutane siku nyingine kwa sababu alikuwa na kazi nyingine hivyo wakapanga kukutana siku nyingine lakini cha ajabu ni kwamba amefariki kabla hata hawajakutana.

download latest music    

Linex anasema “Niliongea na zilla wiki moja kabla na alinitaka tukutane, wiki iliyopita alinipigia tena akaniomba nionane nae alipolakini kutokana na ratiba zangu nilishindwa kukutana nae , sijui alitaka kuniambia nini.Mungu ampumzishe mahali salama. “

Kifo cha msanii huyo kimetia simanzi sana hasa kutokana na kifo chake cha ghafla kilitomuacha kila mtu akishanga.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.