Luis Munana Amsaka Wema kwa Udi na Uvumba

Aliyewahi kuwa mshiriki wa big brother afrika ambae pia aliwahi kuwa mpenzi wa  wema sepetu kabla hajawa na idris sultan amefunguka na kuandika katika ukurasa wake wa instagram kuwa amekuwa akimpigia simu wema sepetu na hata kumtumia ujumbe mfupi lakini hapati  majibu yoyote kutoka kwa mwanadada  huyo.

Luis Munana ambae katika post zake anaonekana kuwepo  Tanzania amekuwa akimtafuta wema kwa udi na uvumba huku akisema kuwa anajua yal yote anayoyapitia lakini anataka kujua anaendelea kwa sababu bado anamjali sana.

download latest music    

katika post hiyo luis aliandika “unapokuwa na mahusiano na mtu siku zote mtaendelea kuwa na mahusiano hata kama mmeachana.hata kama hatuko pamoja lakini bado nakujali na nina amini kuwa huko ulipo huko salama, maana siku zote nimekuwa nikikuwazia mema na nimekuwa nikitaka ufurahi.

ukimya wako umekuwa ukinipa tabu , ninachotaka kujua ni kama uko salama,  @wemasepetu uko wapi na kwanini hujibu whatsappzangu na DMs @martinkadinda kuna nini kinaendelea.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.