Lulu Apanga Kuisaidia Jamii Kwa Kupitia Mavazi Yake

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kuweka wazi mipango yake ya kuuza nguo zake na viatu ambapo pesa atakayoipata itakwenda kusaidia wenye uhitaji katika jamii.

Lulu ambaye Mwanzoni alipanga kugawa nguo na viatu kwa mashabiki zake ameamua kubadilisha na badala yake kuuza mavazi hayo kwa watu na kisha pesa atakayoipata itaelekea kusaidia watu wenye shida mbali mbali.

download latest music    

Lulu amethibitisha hayo katika akaunti yake ya Instagram ambapo amekuja na kitu hicho alichokipa jina la “Save My Valentine”.

Wakati Wengine Tumepata Fursa Ya Kuwa Na Furaha Kwa Vile Tulivyonavyo Kuna Baadhi Ya Wenzetu Wamekosa Nafasi Hiyo….. Na HUU NI MPANGO WA MUNGU?, Kuelekea Siku Ya Wapendanao Februari 14,Nimeamua Kuuza Sehemu Ya Nguo Zangu Ambazo Yawezekana Umeshawahi Kuziona au Haujaziona.
Na Pesa Yote Itakayopatikana Kupitia Mauzo Haya Itaenda Kusaidia Vitu/Watu Wenye Uhitaji Katika Jamii.
Please Join me to Save My Valentine.
#Savemyvalentine”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.