Lulu Apiga Mnada Nguo Zake Kusaidia Wasiojiweza

Msanii wa filamu za Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ameuza  nguo zake kwa nia ya kusaidia watu ambao wanaishi katika mazingira magumu.

 

download latest music    

Siku ya Jumamosi, Januari 26, 2019 Lulu aliwakabidhi nguo  watu walionunua katika zoezi lake la kuuza baadhi ya nguo zake kwaajili ya kukusanya fedha ili kuwezesha project yake ya Save My Valentine, alilolenga kuwasaidia wasiojiweza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na waandishi wa habari, Lulu alisema kuwa kwa siku ile alikabidhi takribani nguo 36 kati ya 40 ambazo tayari zilikuwa zimeshapata wateja na kwamba mwitikio wa zoezi hilo umekua mzuri na unatia moyo kwa sababu watu wamepokea wazo lake vizuri na kumsapoti.

Mimi nina nguo nyingi sana, hivyo nilifikiria baadhi ya nguo kuzigawa bure kwa watu wasiyojiweza, lakini zipo nilizokuwa nikenda nazo kwenye events na shoo, nikaja na wazo baada ya kuona bora niziuze ili nipate pesa ya kuwasaidia watu wasiyojiweza ambao kwangu mimi nitasherehekea nao Siku ya Wapendandanao kama Valentine wangu, Februari 14.

Zoezi bado linaendelea, nitaposti tena jumatatu na watu wanaohitaji tutawasiliana ili wanunue. Ninafanya hivi kwa sababu nataka siku moja nikiondoka duniani niache alama ya mazuri niliyofanya, nimefanya mabaya mengi, nimepitia magumu mengi katika maisha yangu, lakini sasa hivi ni wakati wa kufanya angalau mema ili siku moja nikumbukwe kwa hiki ninachiokifanya”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.