Lulu Diva Adai Akikumbuka Alivyokuwa Video Queen Anatamani Kulia

Msanii wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa piga ya garagaza hawezi kuwa video queen tena  kwenye video za wasanii wengine.

Lulu Diva ni moja kati ya wasanii ambao kusema ukweli wametoka mbali kwani alianza kama muuza mgahawa baadae akaingia kwenye ulimwengu wa sanaa kama video vixen kwenye video za wasanii mbali mbali na mpaka sasa anafanya vizuri.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Vibes, Lulu Diva amesema  kwamba akikumbuka baadhi ya mambo kwenye u-video queen, muda mwingine hutamani hata kulia.

Kiukweli sitaki kusikia kabisa kuhusu mambo ya u-video queen, ni kweli ni mapito yangu na ndiyo huko nilikotoka, lakini kwa sasa ninaendelea na kuweka akili yangu yote kwenye muziki ninaoufanya na uigizaji huko ndiko ninafikiria zaidi.

Mtu unachukuliwa na kupewa kazi ya kupamba wimbo wa mtu kwa malipo kidogo, bado hicho kidogo chenyewe unakihangaikia na manyanyaso kibao”.

Wasanii wengi ambao waliwahi kuwa video queens kama vile Gigy Money na Amber Lulu wameponda sana kazi hiyo kusema haina pesa kabisa yaani wanaishia kupewa pesa ya nauli.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.